January 29, 2016

ABAJALO

Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) mzunguko wa pili unatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, kwa timu nne za juu kutoka makundi A, B, C na D kusaka kupanda daraja msimu ujao.

Kundi A, michezo mitatu itachezwa ambapo Green Warriors watacheza dhidi ya Mvuvuma, Abajalo watawakaribisha Mirambo FC uwanja wa Ali Hassani Miwnyi Tabora, huku Transit Camp wakicheza dhidi ya Singida United uwanja wa Kambarage siku ya Jumapili.

Kundi B, Madini FC watakua wenyeji wa Alliance FC uwanja wa Mbulu, AFC Arusha watacheza dhidi ya Pamba uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha siku ya Jumapili, huku Bulyanhulu FC wakiwakaribisha JKT Rwamkoma siku ya Jumatatu uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Kundi C, Leo Ijumaa Cosmopolitan watacheza dhidi ya Kariakoo uwanja wa Karume, Changanyikeni dhidi ya Mshikamano uwanja wa Karume siku ya Jumatatu, huku Abajalo wakicheza dhidi ya Villa Squad siku ya Jumanne.


Kundi D, Jumamosi Mbeya Warriors watacheza dhidi ya Sabasaba uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mighty Elephant watacheza dhidi ya Mkamba Rangers siku ya Jumapili uwanja wa Majimaji mjini Songea, huku African Wanderes wakiwakaribisha Wenda FC uwanja wa Wambi Mafinga siku ya Jumatatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic