January 29, 2016

MAREHEMU SWAI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapenda kuwajulisha wapenzi, wadau, wa mpira wa miguu nchini kuwa, mwili wa aliyekua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai utaangwa leo saa 9 alasiri katika hosiptali ya Muhimbili, na baadae saa 11 jioni itaanza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika leo Ijumaa saa 9 alasiri katika hospitali ya Muhimbili, ambapo ndugu, jamaaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu watapana nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Epaphra Swai, na baadae majira ya saa 11 jioni itaanza safari ya kuelekea Machame mkoani Kilimanjaro.

Mazishi ya marehemu Epaphra Swai yatafanyika kesho Jumamosi mchana nyumbani kwako Machame Kilimanjaro.

TFF inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu pamoja na familia ya marehemu, na kusema wako pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo ya msiba huo.

Marehemu Epaphra Swai alifariki dunia jana asubuhi katika hospital ya taifa ya Muhimbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic