January 27, 2016


Balaa kubwa limeikumba Yanga ambayo hivi sasa ipo katika maandalizi makali ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza wikendi ijayo baada ya wachezaji wake kushindwa kufanya mazoezi.

Timu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 39, imekumbwa na balaa la nyota wake 11 wa kutumainiwa kuwa nje ya uwanja wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Hali hiyo imeonekana kuwachanganya vilivyo viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Wachezaji hao ni Amissi Tambwe, Simon Msuva, Malimi Busungu, Vincent Bossou, Boubacar Garba, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na  Juma Abdul.

Kwa pamoja nyota hao jana hawakuweza kufanya mazoezi na timu hiyo ambayo kwa sasa inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Akizungumzia hali hiyo Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, alisema kuwa anajitahidi kadiri ya uwezo wake kuhakikisha nyota hao wanarejea kikosini mara moja.

“Nikweli kabisa wachezaji hao hawapo vizuri kiafya lakini tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha wanakuwa sawa.


“Hata hivyo, Twite, Juma, Bossou na Msuva kesho (leo), wanaweza kuungana na wenzao kwa ajili ya mazoezi hao wengine waliobaki kama mambo yatakwenda vizuri basi watarejea uwanjani baada ya muda mfupi,” alisema Matuzya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic