January 28, 2016


Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema samahani sana Watanzania kwa kuiruhusu Azam FC kwenda kwenye “Bonanza” la Zambia, wakati Ligi Kuu Bara inaendelea.

Malinzi amesema wakati TFF inatoa ruhusa kwa Azam FC, yeye alikuwa nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Malinzi amekiri jambo hilo kuwa si sahihi, ndiyo maana ameamua kuwa muungwana.

“Kweli naomba radhi kutokana na hili la Azam FC, ila wakirudi watakuwa kwenye kipindi kigumu,” alisema na kuongeza.

“Watalazimika kucheza mara mbili kwa wiki, Jumatano na Jumamosi ili wamalize mechi na kulingana na wenzao,” alisema.

TFF imezua zogo na gumzo baada ya kuiruhusu Azam FC kwenda Zambia ikiwa ni baada ya kucheza mechi tat utu, tokea mapumziko ya Kombe la Mapinduzi.

Jana Katibu Mkuu TFF, Mwesigwa Celestine alionekana kujichanganya baada ya kusema bodi ya ligi walisema hawana shida Azam FC kuruhusiwa kwenye kushiriki bonanza la Zambia.


Lakini Bodi ya Ligi, nao nao wakasisitiza kwamba Azam waliomba ruhusa muda mwingi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic