January 7, 2016



Mashabiki wa Yanga wanajua kama kikosi chao kitayumba leo katika mechi dhidi ya Mtibwa usiku, safari imewakutana.

Bahanuzi alikuwa shujaa baada ya kuisaidia Mtibwa Sugar kupata pointi tatu kwa kuilaza Mafunzo kwa bao 1-0 katika michuano hiyo ya mapinduzi.

Mashabiki hao waliotuma maoni katika email ya www.salehkubwa@gmail.com, wamemtaka Kocha Hans van der Pluijm kutowadharau mshambuliaji Said Bahanuzi na mwenzake Hussein Javu.

"Pluijm ajue Bahanuzi anacheza kwa mkopo Mtibwa, lazima atataka kutufunga ili arudishwe. Akifanya hivyo sisi tutaumia sana, hivyo awekewe ulinzi haswa," alisema Said Majani aliyesema anatokea Ilala, Dar es Salaam.

Humfrey John wa Tunduma, Mbeya ameandika: "Tukifungwa na Bahanuzi, nitaumia sana. Hata yule Javu, tayari ameanza tambo. Ninajua atataka kuonyesha Yanga walimuondoa kwa kumuonea. Kwa kweli nna hofu sana."

Mashabiki hao walionyesha kuwa na hofu na kikosi chao kuhofia kitapoteza mechi ya leo dhidi ya Mtibwa Sugar, basi Azam FC na Mtibwa zinaweza kupata nafasi ya kwenda nusu fainali.

Tayari Yanga ina pointi nne huku Azam FC ikiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare mbili dhidi ya Yanga na Mtibwa Suga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic