January 5, 2016



Kocha Mecky Maxime anaamini kikosi chake kitafanya vizuri zaidi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, licha ya mwamuzi msaidizi katika mechi yao dhidi ya Azam FC ‘kuwauma’.

Maxime amesema hawajakata tamaa, pia umma umeona kilichotokea katika mechi yao iliyosha kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

“Kila mtu aliona, hatuna haja ya kuendelea kulalamika na sasa tunaelekeza nguvu katika mechi zetu nyingine kwa lengo la kufanya vizuri,” alisema Maxime.

Kabla ya hapo, Maxime aliwaonya waamuzi kuachana na tabia ya upendeleo ambayo itaharibu maana na utamu wa mashindano hayo.

Mtibwa Sugar walilalmikia bao lao lililofungwa na Ramadhani Kichuya dakika za mwisho za mchezo, lakini mwamuzi huyo mwanamama akainua kindendera. Hali iliyosababisha aondoke uwanjani akisindikizwa kwa ulinzi wa askari polisi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic