January 21, 2016


Kocha Jackson Mayanja wa Simba, amesema bao la Dani Lyanga litamsaidia kurejesha hali ya kujiamini na kucheza vizuri zaidi.

Lyanga alifunga bao la pili wakati Simba ikiimaliza JKT Ruvu kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jana.

Mayanja amesema Lyanga ni mchezaji mzuri lakini kuna wakati wachezaji hutokewa na mambo ya kisaikolojia.

"Kufunga kutamsaidia kurejesha hali ya kujiamini, baada ya hapo ataanza kurudi na kucheza vizuri zaidi, lazima tukubali kumpa muda," alisema.

Lyanga alianza kwa kasi ndani ya kikosi cha Simba, lakini baadaye alianza kuonekana kupoteza hali ya kujiamini.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic