January 24, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema mshambuliaji Hamisi Kiiza ataendelea kufanya vizuri kwa kuwa ana kipaji cha juu cha umaliziaji.

Kiiza alipiga mabao mawili mjini Morogoro, jana na kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burkina Faso ya mjini humo katika mechi ya Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam Sports.

Mayanga amesema kinachoweza kumzuia Kiiza kufanya vema, labda majeraha lakini kama atakuwa fiti, ana nafasi nzuri ya kuwa msaada mkubwa Simba.


“Kiiza ni mzoefu, pia ana kipaji cha ufungaji. Anajua afanye nini anapokaribia langoni, ndiyo maana nasema ana nafasi kubwa ya kufanya vema,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic