January 24, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, alimkaribisha kiungo wake, Haruna Niyonzima kwa bashaha kuu.

Pluijm raia wa Uholanzi alionekana kumfurahia Niyonzima wakati akirejea mazoezini kwa mara nyingine tena baada ya kuwa amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa wachezaji na makocha wa Yanga kumuona Niyonzima akirejea na kuanza mazoezi.


Yanga inashuka dimbani leo kuwavaa Friends Rangers kuwania Kombe la FA kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tu baada ya watani wao Simba kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Burkina Faso ya mjini Morogoro.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic