January 22, 2016


KABLA YA KUTEREMKA KWENYE GARI, MSUVA TAYARI ALIKUWA TAYARI KUMKARIBISHA NIYONZIMA...

Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzoma amerejea kundini leo na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wachezaji wenzake.

Simon Msuva alikuwa mtu wa kwanza kumpokea Niyonzima raia wa Rwanda bado akiwa ndani ya gari lake na baadaye akaungana na wengine wakiongozwa na Salum Telela, Mustapha Ally ‘Barthez’ pamoja na kocha wa makipa, Juma Pondamali, wote wakionyesha kuwa na furaha kuu.

Niyonzima alisimamishwa kwa utovu wa nidhamu, lakini uongozi Yanga kupitia kamati ya utendaji makini baadaye uliamua kumrejesha alipomba radhi na kubaini ndani ya sakata lake kuna mambo hayakuwa yameenda sawa.


MSUVA ANAZIDI KUMKARIBISHA TENA....



PONDAMALI ALISHINDWA KUJIZUIA... 
FURAHA YA TELELA....

1 COMMENTS:

  1. Kitu pekee ninachokiona na ambacho nadhani ndo siri ya timu kufanya vizuri ni upendo!! Inaonekana timu wanaishi kama familia which is good

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic