January 28, 2016

NONGA KAZINI

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Paul Nonga sasa anaelewa tofauti ya klabu kubwa kama Yanga na zile alizotoka kama Mbeya City na Yanga.

Nonga ambaye tayari ameanza kuonyesha makali akiwa na Yanga, amesema mshambuliaji wa Yanga anakabwa kwa juhudi kubwa na mabeki.

“Kila mechi unayoichezea Yanga ni ngumu na unatakiwa kujituma zaidi. Mabeki wanakukaba kwa juhudi na kupania sana,” alisema.

“Naona ni tofauti kabisa, lakini naelewa kwa kuwa niko timu kubwa. Nitaendelea kujituma na kushirikiana na wenzangu.”


Nonga aliyewahi kuzichezea Mbeya City na Mwadui FC ni kati ya mafowadi Watanzania wenye uwezo mkubwa wa kupachika mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic