January 30, 2016

KIONGERA

Mambo sasa safi Simba kwani majeruhi Mohammed Fakhi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Paul Kiongera wapo vizuri na watarejea kikosini kuanzia keshokutwa Jumatatu.

Fakhi na Tshabalala walikuwa wakisumbuliwa na goti wakati Kiongera raia wa Kenya yeye anasumbuliwa na nyama za paja.

Kwa mujibu wa daktari wa Simba, Yassin Gembe, wachezaji hao wanatia faraja kutokana na maendeleo mazuri katika majeraha yao na mambo yakienda sawa, watarejea uwanjani kuanzia Jumatatu ijayo.

Fakhi aliumia kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Tshabalala aliumia katika mechi na maafande hao na Kiongera alishtua nyama za paja mazoezini.


“Tshabalala yeye anahudhuria kliniki kila siku na anatarajia kumaliza matibabu Jumamosi (leo), Fakhi naye yupo vizuri wiki ijayo atarudi uwanjani. Kiongera kwa kuwa tulimuwahi mapema kumpa matibabu, naye anaendelea vizuri na anaweza kurejea mapema zaidi,” alisema Gembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic