January 30, 2016

MWAMBUSI

Kiungo Thabani Kamusoko na mastraika Amissi Tambwe na Donald Ngoma wa Yanga, wamepewa kazi maalumu ya kutoa pasi za mwisho na kufunga mabao katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwabusi, jana asubuhi katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani, alionekana akitumia muda mwingi kuwaelekeza Kamusoko, Tambwe na Ngoma namna ya kutoa pasi za mwisho na kufunga.

Mbali na wachezaji hao, pia mabeki wa pembeni Oscar Joshua na Juma Abdul walipewa kazi ya kutafuta na kuokoa mipira ya pembeni kikamilifu huku wakipiga krosi zenye macho langoni.

Mwambusi alifanya hivyo huku muda mwingi akielekeza matumizi ya pasi ndefu kutokana na hali ya uwanja huo kuwa si rafiki wa pasi fupifupi. 

Katika mazoezi hayo, Kamusoko alifunga mabao mawili huku Tambwe na Ngoma wakionekana kutokuwa makini katika kulenga lango kwani mipira waliyopiga mingi ilitoka nje ya lango au kugonga mwamba.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Plujim alionekana kuwa ‘siriazi’ akiwaelekeza wachezaji wake kucheza soka la haraka na matumizi ya pasi ndefu.

“Angalieni msitulize mipira ya chini sana uwanja huu mipira haitulii mguuni, mtapoteza pasi nyingi,” alisikika Pluijm akiwaeleza wachezaji wake.


Uwanjani hapo, leo Yanga inacheza na Coastal Union katika Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic