January 29, 2016


Mshambuliaji hatari na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta sasa ni mali ya KRC Genk ya Ubelgiji, rasmi ameondoka TP Mazembe.

Leo, Samatta amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kuichezea Genk ambayo inapambana katika Ligi Kuu Ubelgiji.

Kupitia mtandao wa kijamii kwenye ukurasa wake wa Instagram, Samatta amewashuruku wachezaji wa TP Mazembe kwa ushirikiano, lakini amemshukuru tajiri Moise Katumbi.

“Ahsante kwa bosi wangu Katumbi kwa fursa ya kucheza ndani ya TP Mazembe hadi leo, Kocha, wachezaji wenzangu, mashabiki na viongozi wote, muda wote wamenipa support.


“Napenda kuwataarifu, sasa rasmi nimekuwa mchezaji wa KRC Genk,” aliandika Samatta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic