January 28, 2016


Nahodha wa Yanga, Nadir Ally ‘Cannavaro’ anatarajia kurejea uwanjani Jumatatu ijayo na kufanya mazoezi pamoja na wenzake.

Cannavaro amekuwa majeruhi kwa takribani miezi miwili sasa baada ya kuumia wakati akiitumikia timu ya taifa, Taifa Stars.

Lakini taarifa zimeeleza ameishaanza mazoezi mepesi pamoja na kufanya mazoezi ya gym pamoja  na kukimbia taratibu.


Daktari wa Yanga,  Nassor Matuzya naye amesema ni baada ya siku chache, Cannavaro ataungana na wenzake.

“Kweli hali yake imaimarika, kama mambo yatakwenda hivi tuna matumaini makubwa ataungana na wenzake wiki ijayo,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic