January 28, 2016


Kikosi cha Yanga, kimeondoka leo alfajiri jijini Dar es Salaam na kikosi kizima kwenda mjini Tanga kwa ajili ya mechi yao dhidi Coastal Union.

Yanga imeondoka kimyakimya kwenda Tanga baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilipanga kuikatalia kwenda Afrika Kusini, tena katika dakika za mwisho.

“Kweli Yanga wameondoka, wamekwenda na kikosi kizima Tanga. Unajua kuna figisu ya hili suala la Azam FC kuruhusiwa kwenda Zambia wakati ligi inaendelea.

“Yanga nao walitaka kwenda Afrika Kusini. Lakini kukawa na taarifa kuna mchezo ungechezwa, Yanga wameshituka na kuondoka kimyakimya,” kilieleza chanzo.

Hakuna kiongozi wa Yanga aliyekuwa anapokea simu kuthibitisha kuhusu kuondoka kwa timu hiyo pamoja na hizo figisu.

Lakini ripota wa Salehjembe akathibitisha kuliona basi la Yanga likichanja mbuga kwenda Tanga alfajiri ya leo.


“Ndiyo, Yanga wamepita leo asubuhi. Basi lao limepita mkwaju ile mbaya, tukawa tunajiuliza kama ile safari yao ya Sauz wameahirisha au ipo,” alisema ripota huyo wa mkoani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic