January 26, 2016


Kiungo nyota wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho yuko nchini India ambako amezua tafrani kubwa kutokana na mashabiki wengi kujitokeza kumlaki.

Taarifa zimekuwa zikieleza yuko nchini India kwa ajili ya mapumziko, lakini alihusika na kuzindua filamu ya katuni mwenye mwonekano kama Ronaldinho.

Wakati akiwa njiani kwenda hotelini, alinusurika na ajali baada ya taa ya barabarani kuanguka hatua chache kutoka lilipokuwa gari lake.

Ilielezwa taa hiyo ilianguka baada ya wananchi katika enero la Kerala kuiparamia wakitaka kumwona.

Muda mwingi askari polisi walilazimika kutumia nguvu ya ziada ili kuhakikisha anapita na kufika sehemu anayokwenda kutokana na mashabiki wengi kutaka kumuona nyota huyo wa zamani pia wa timu ya AC Milan na timu ya taifa ya Brazil.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic