January 25, 2016


Straika Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe, amejiweka sokoni kwa kusema kuwa ataitumia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kujitangaza.

Tambwe, raia wa Burundi, amesema atahakikisha anajituma kijeshi katika michuano hiyo ili kuwavutia mawakala mbalimbali.

Yanga inatarajiwa kukutana na Cercle de Joachim ya Mauritius Februari 14 katika michuano hiyo.

Tambwe ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 13 na atataka kuonyesha uwezo wake hata kwenye michuano ya kimataifa.

“Nimejiandaa vyema kwa ajili ya kuisaidia timu yangu ya Yanga katika michuano ya klabu bingwa, kuhakikisha tunaweza kufanya vyema ili kusonga mbele.

“Hiyo ni nafasi ya kipekee kwangu kuonyesha uwezo ili kupata soko kwani michuano hiyo inafuatiliwa sehemu mbalimbali, lengo langu ni kupiga hatua zaidi kisoka, ndiyo maana huwa najituma kuhakikisha nafikia malengo.


“Ili malengo yangu yatimie ni vyema nikajituma kwenye ligi na katika klabu yangu kwa ujumla,” alisema Tambwe.

1 COMMENTS:

  1. Tambwe namuogopa maana utadhani mchawi,mara nyingi akisema atafanya kitu kweli kinafanyika,
    aliapa kuifunga simba na kweli akafunga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic