SHEVA (WA KWANZA KULIA, MSTARI WA MBELE) AKIWA NA KIKOSI CHA TOTO AFRICAN. |
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana mwishoni mwa wiki na kupitia kesi, mashauri mbalimbali kuhusiana na usajili na mikataba ya wachezaji na viongozi mbalimbali chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Mandi.
AFRICA LYON dhidi ya Wachezaji
i. Morris Kaniki-Mwadui
ii. Miraji Athuman-Toto Africans na
iii. Emmanuel Simwanda-Mwadui
Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji imeamua klabu husika ziandikiwe barua ya kumalizana na African Lyon na wapewe wiki mbili toka tarehe 15.01.2016 hadi tarehe 30.01.2016 kama watashindwa kumalizana watasimamishwa kuzichezea klabu hizo.
Wakimalizana wapewe barua na African Lyon ndiyo itakayotuma barua TFF kuwaruhusu waendelee kucheza.
KESI MBALIMBALI ZA MADAI YA WACHEZAJI NA WALIMU
i. Kesi namba moja kati ya Fadhil Msemi anayewawakilisha wachezaji 28 wa KMC wanaodai malipo ya mishahara yao kwa mwajiri wao KMC
Kamati imeamua mwakilishi wa wachezaji ndugu Fadhil Msemi akae na viongozi wa KMC, katibu wao na mratibu wa timu wajadili na kupitia utaratibu wa malipo namna viwango vya malipo kwa wachezaji hao vinavyopaswa kuwa na iwasilishwe TFF Jumatatu.
ii. Kesi namba mbili ilikuwa kati ya Stand United dhidi ya wachezaji na wataalamu wake wanaoidai. Stand United iliwakilishwa na Ernest Brown kwa barua kwa hiyo maamuzi yote ya Kikao yatakuwa halali.
Kesi zilizojadiliwa zilikuwa ni kama ifuatavyo.
a. Kesi ya madai ya Mchezaji Peter Mutabuzi aliyeichezea Stand United dhidi ya klabu yake, Mutabuzi aliwakilishwa na kiongozi wa klabu yake ya sasa Frank Mchaki wa KMC.
Mchezaji huyu alikuwa anaidai klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 3,400,000/= lakini kikao kilikubaliana alipwe kiasi cha Tsh 2,000,000/= ndani ya mechi nane za ligi toka tarehe ya kikao 15.01.2015.
b. Kesi kati ya Ndikumana Hamad dhidi ya Stand United, mwenyewe alikuwepo na pia aliwakilishwa na Fadhil Hussein. Ndikiumana anaidai klabu ya Stand malimbikizo ya mshahara, malazi na chakula kiasi cha shilingi 11,025,000/=. Wamekubaliana mchezaji anarudishwa kwenye klabu yake ya Stand United kuitumikia na pia madai yake watamalizana huko Stand na pia Stand imlipie gharama alizokuwa anaishi akiwa Dar es Salaam hotelini maana mchezaji sio raia wa Tanzania.
c. Ben Kalama ambaye alikuwa kocha wa makipa wa Stand United alikuwa anadai malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Tsh usd 1,350 aliwakilishwa na Fadhili Hussein yeye walikubaliana kuwa anarudishwa kwenye timu na watalipana huko huko madai yake. Kuhusu madai yake kiasi cha dola 1,350 kamati iliamua kwa kuwa ni madai halali na mwakilishi amekiri hilo basi wakatwe kwenye vyao vya mapato na TFF.
d. Mathias Lule dhidi ya Stand ya madai ya mishahara, posho na medical insurance kiasi cha Tsh 48,300,000/= aliwakilishwa na Fadhil Hussein. Ilikubaliwa ya kwamba alipwe kiasi cha usd 4,300.00 ambacho kimethibitishwa na kukubaliwa tayari na juu ya madai mengine watakaa na muajiri wake wa zamani na kuyajadili kuona namna ya kulimaliza suala hili. Fedha hiyo itakatwa kwenye vyanzo vyao vya mapato.
e. JAKI FOOTBALL ACADEMY dhidi ya Stand United kiasi cha shilingi 7,600,000. Jaki waliwakilishwa na Fadhil Hussein ambaye alisema deni wanaloidai Stand United ni kiasi cha Tsh 4,200,000/= na deni hili limekubaliwa na litalipwa na Stand United kwenye vyanzo vyao vya mapato toka TFF.
f. Muhibu Kanu dhidi ya Stand United anayeidai mishahara, na posho klabu ya Stand United kiasi cha Tsh 16,600,000/=. Makubaliano yamefikiwa kweli Muhibu anaidai Stand kiasi hicho na ameshaanza kulipwa kupitia Bodi ya ligi kiasi cha Tsh 2,600,000/= hivyo kiasi kilichobakia cha Tsh 14,000,000/= anaenda kujadiliana na muajiri wake kwa kuwa amerudishwa kazini.
g. Kesi kati ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Stand United Emmanuel R. Massawe dhidi ya Stand United anayeidai Klabu ya Stand United kiasi cha Sh 12,100,000/= imehairishwa kwa kuwa muhusika hakuwepo wala hakutuma muwakilishi.
3. Kesi namba tatu ilikuwa ni kati ya Ndanda Fc dhidi ya wachezaji wake wanaoidai timu hiyo. Kesi hii ilishindwa kusikilizwa kwa kuwa wachezaji na wawakilishi wa wachezaji walikuwepo lakini klabu ya Ndanda FC haikutuma mwakilishi pamoja na kuletewa mwaliko siku ya tarehe 12/1/2016.
Hivyo kamati iliamua yafuatayo
a. Ndanda FC ikatwe kwenye vyanzo vyao vya mapato kiasi cha madai yaliyothibitishwa na mwakilishi wao katibu mkuu kwenye kikao kilichopita ambayo yalikuwa ya wachezaji wawili Rehani Kibingu kiasi cha tsh 2,000,000/= na Meshack Wilfredy Meshack aliyekuwa pia anadai kiasi cha Tsh 2,000,000/=.
b. Pamoja na katibu kuahidi kuleta ufafanuzi wa madai ya baadhi ya wachezaji tarehe 28.12.2015 kwa barua TFF mpaka kikao cha tarehe 15.01.2016 hakuwa ameleta barua yoyote na timu haikuleta mwakilishi kwenye kikao hicho hivyo basi kamati inaiagiza sekretarieti ya TFF kuwaandikia barua kutaka kujua ufafanuzi wa madeni ya wachezaji
i.Said Mketo anayedai Tsh 2,720,000/=
ii.Saleh Malande anayedai Tsh 2,000,000/=
iii.Rajab Isihaka anayedai kisai cha 3,720,000/= na pia kamati inataka kujua ni namna gani klabu ya Ndanda FC itawalipa wachezaji hao wanaoidai.
c. Kamati pia ilihakikishiwa na muwakilishi wa wachezaji ya kwamba wachezaji Mohamed Upatu na Amir S. Msumi waliokuwa wanaidai klabu hiyo kiasi cha Tsh 2,600,000/= kila mmoja hawaidai tena klabu hiyo na walishamalizana nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment