January 28, 2016

MAYANJA
Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amesema atatoa nafasi kwa kila mchezaji atakayejituma.

Mayanja amesema kila atakayejituma, ana nafasi ya kuitumikia timu hiyo na kuisaidia.

“Katika kazi kila mtu anakuwa na uwezo tofauti, lakini suala moja linakuwa muhimu kwa kila mmoja; kujituma,” alisema.

“Unaweza kuwa na kipaji, halafu ukashindwa kufanya vizuri kama hauna juhudi. Ninaamini wachezaji wote wa Simba lengo lao ni kufanya vizuri.

“Kwangu nataka kutoa nafasi kulingana na wakati, lakini suala la kujituma kwa manufaa ya klabu ni muhimu.”
Kocha huyo Mganda ameiongoza Simba katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na moja ya FA Cup inayodhaminiwa na Azam Sports na zote ameshinda.


Mayanja amechukua nafasi ya Mwingereza Dylan Kerr ambaye sasa tayari yuko nchini Afrika Kusini inakoelezwa kuwa anasaka timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic