January 6, 2016


Uongozi wa Yanga upo kwenye hatua za mwisho za kwenda nchini Misri zilizopo ofisi za Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya kujua jinsi gani ya kuliondoa jina la aliyekuwa kiungo wako Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Hiyo ni siku chache tangu viongozi wa timu hiyo walipotuma majina ya wachezaji wao watakaowatumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa itakayofanyika mwaka huu.

Niyonzima hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa kile kilichodaiwa ni utovu wa nidhamu aliounyesha.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa jina la kiungo huyo lilifika Caf kabla ya uongozi wa Yanga kumchukulia hatua za kinidhamu za kumsitishia mkataba wake Niyonzima kwa kitendo hicho cha kinidhamu.

Muro alisema, Kamati ya Utendaji ya Yanga imepanga kukutana kwa ajili ya kujadiliana suala hilo ikiwemo jinsi ya kwenda kulitoa jina la kiungo huyo ambaye ni nahodha wa Rwanda.

Aliongeza kuwa, mara baada ya kamati hiyo kukutana na kujulikana hatma ya kiungo huyo haraka watapeleka taarifa Caf na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Naomba nikiri kabisa ni kweli jina la Niyonzima tulilituma Caf, lakini tulilituma jina hilo kabla ya kumchukulia hatua ya kinidhamu ya kuusitisha mkataba wake wa kuichezea Yanga.

“Hivyo, Kamati ya Utendaji ya Yanga imepanga kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kujadiliana suala hilo ikiwemo kujua jinsi ya kulitoa jina hilo la Niyonzima katika usajili wetu wa Caf.


“Mara baada ya kikao kufanyika haraka tutapeleka taarifa za kiofisi Caf na TFF ambao wanasema kuwa wanamtambua Niyonzima ni mali yetu tukiwa tumeusitisha mkataba wake,” alisema Muro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic