January 29, 2016

AY

Gumzo kubwa katika muziki kwa sasa ni video ya AY ambayo imeangaliwa na watu zaidi ya milioni moja, siku chache tu baada ya kuwa imetupiwa mtandanoni.

Hiyo ni video ya rapa anayebeba heshima kubwa kwa kutengeneza njia iliyoupeleka muziki wa Bongo Flava kimataifa, AY ametoa video ya remix ya single yake Zigo aliyomshirikisha mshindi wa Best Worldwide Act Africa/India kwenye tuzo za MTV EMA 2015, Diamond Platnumz.

Kazi hiyo inayotarajiwa kufuata mafanikio ya kazi zake za kimataifa zilizopita, zikiwemo ‘Touch Me Touch Me’ aliyomshirikisha Sean Kingston na Ms Triniti pamoja na ‘Speak With Your Body’ aliyowashirikisha Romeo na Lamyia Good wa nchini Marekani.

Katikati ya Desemba mwaka jana, rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Ambwene Allen Yesayah aliungana na Diamond nchini Afrika Kusini kutengeneza video ya wimbo huo na kumtumia muongozaji mahiri Alessio Bettocchi wa kampuni ya Studio Space Pictures.

Kampuni hiyo si ngeni katika kutengeneza video za viwango vya juu za wasanii wenye majina makubwa Afrika ikiwemo Show ya Victoria Kimani, The Saga ya Anati, Sim Dope ya AKA, Asanteni kwa Kuja ya Mwana FA na nyingine nyingi.

AY

AY anasema ameamua kufanya video Zigo Remix kwakuwa mwaka 2016 ameamua kutambulisha mfumo mpya wa ufanyaji kazi kwenye muziki wa Bongo Flava katika upande wa video, anaoamini utaleta mapinduzi mengine kama aliyoyafanya enzi ameanza kutoka nje ya nchi kufanya video zake na kutafuta collabo za kimataifa zilizofanikiwa.

Rapa huyo amedai aliamua kumshirikisha Diamond kwenye Zigo Remix kwakuwa ameona ni vema kumshirikisha Mtanzania mwenzake ili kuupa nguvu muziki wa Bongo Flava bila kutegemea nguvu ya msanii wa nje.

“Hiyo ni ishara tu ya kuonyesha kuwa tunaweza tukafanya kitu sisi wenyewe Watanzania au watu wa Afrika Mashariki wenyewe lakini tunaweza kutengeneza muziki mkubwa kama wanavyofanya wengine,” anasema AY.

AY

Zigo imebaki kuwa na mdundo ule ule mtamu na wa kuvutia alioufanya mtayarishaji aliyepika hits nyingi mwaka 2015, Nahreel lakini sauti za Zigo Remix zimesimamiwa na Hermy B wa B’Hits Music Group.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic