February 15, 2016


Mashabiki wa Bastia ya Ufaransa wamezua sekeseke ikiwa ni pamoja na kushambulia kituo cha Polisi cha mji wa Bastia,.

Licha ya timu yao kushinda, mashabiki hao walifanya vurugu na wenzao wakakamatwa na askari polisi.


Lakini mashabiki hao walionekana kupinga suala hilo na kutaka wenzao waachiwe kwa nguvu tena mara moja.

Walipoona jambo hilo halitekelezwi, walipambana kwa kuvamia kituo cha polisi cha Bastia na inaelezwa askari mmoja aliumizwa kichwani.

Vurugu zilikuwa kubwa, huku mashabiki hao wakiunguza baadhi ya sehemu. Baadaye walivunja vioo vya magari pamoja na kuyaunguza mengine.

Baadaye polisi walivamia eneo hilo na kuwakamata baadhi waliokuwa wamefunika nyuso zao.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic