February 25, 2016

 
MURO
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekana kumtukana Msemaji wa Simba Haji Manara na kusema kila anachosema ni kweli tupu.

Manara amefanya kikao na waandishi wa habari leo na kutishia kumfikisha Muro polisi na ikiwezekana mahakamani kutokana na kumdhalilisha huku TFF ikionekana kulifumbia macho suala hilo licha ya yeye kuwasilisha malalamiko yake.

Kwa upande wa Muro amekana tuhuma hizo kuwa alimtukana Manara na kuidhalilisha klabu ya Simba.

Muro akamtaka Manara kuchukua hatua kwani vyombo vya dola kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mahakamani ama polisi kuliko kupiga ‘porojo’.


“Kwani ni uongo kusema kocha wao amekuja kwa basi na wetu amekuja kwa ndege? Si wamemsajili kutoka Coastal pale Tanga na wetu ni Mholanzi amekuja kwa ndege. Kama amaamini amedhalilishwa aende kwenye vyombo vya dola akashtaki,” alisema Muro.

1 COMMENTS:

  1. Manara kama hataki kutaniwa basi ahamie ndanda au majimaji!! Timu inapokuwa haifanyi vizuri ni kawaida kupewa majina!! Amesahau juzi tu haoa Yanga waliitwa ndala mara Yeboyebo nk!? Hiyo iwe ni nguvu ya kuifanya timu ifanye vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic