Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema anawasubiri kwa hamu Azam ili awaonyeshe kazi watakapokutana Jumamosi hii.
Yanga na Azam zinatarajiwa kupambana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo kwa sasa Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 46, ambazo ni sawa na Azam, lakini wametofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Cannavaro, tangu aumie kisigino Novemba, mwaka jana, hakuonekana uwanjani kwa muda mrefu mpaka hivi karibuni alipocheza dhidi ya JKT Mlale kwenye mchezo wa Kombe la FA ambapo Yanga ilishinda 2-1 na kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.
“Tayari nimepona kabisa na kwa sasa naweza kucheza, sasa nguvu zangu nimezielekeza kwa Azam ambao tutapambana nao kwenye ligi hivi karibuni, nimejipanga kuwanonyesha kazi kwani tumedhamiria kushinda mchezo huo ili kuutetea ubingwa wetu,” alisema Cannavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment