Kocha wa timu ya taiga ya Brazil, Carlos Dunga amesema mshambuliaji wake nyota, Neymar hana uhakika kama atacheza katika michuano ya Copa America itakayofanyika Marekani.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika Juni na Brazil ipo Kundi B na timu za Ecuador, Haiti na Peru.
“Hapa ni suala la kuzungumza na Neymar mwenyewe, kama yuko tayari au vipi. Ukiniuliza mimi tu, ntakuambia nataka acheze,” alisema Dunga, kiungo wa zamani wa Brazil.
Kwa kipindi hiki Neymar anaonekana kuwa busy na majukumu ya kikosi cha timu yake ya Barcelona.








0 COMMENTS:
Post a Comment