Mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera ambaye alikuwa majeruhi hadi kurudi kwao Kenya, sasa yuko kamili.
Kiongera amerejea na kuungana na kikosi cha Simba, sasa yuko tayari kuongeza nguvu.
“Kweli Kiongera amerejea na yuko tayari kuungana na wenzake kwa ajili ya kuongeza nguvu,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.
“Unajua Kiongera amekuwa akisumbuliwa na majeruhi kila mara, lakini sasa yuko vizuri tu.
“Tunajua hatafanya vizuri ndani ya siku chache. Lakini atakuwa msaada tu,” aliongeza.
Simba iliwahi kumtoa mkopo kwa kumrejesha kwao Kenya mara baada ya kuumia katika mechi ya kwanza tu ya ligi msimu uliopita.
Aliporejea msimu huu wakati wa dirisha dogo, bado hakuweza kuonyesha cheche zake.







0 COMMENTS:
Post a Comment