MPIRA UMEKWISHAAA
GOOOOOOOOOOO Dk 90+3.14 Msuva anaifungia Yanga bao la nne baada ya kupokea pasi nzuri kabisa ya Deus Kaseke aliyepewa pasi na Paul Nonga
Dk 90+1 shuti kali la Abdrahman Mussa baada ya kupokea pasi ya Dilunga linagonga mwamba na kutoka nje
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, krosi safi ya Juma Abdul inatua kichwani mwa Nonga, lakini anashindwa kulenga
Dk 88, Msuva anapata pasi safi akiwa ndani ya eneo la 18, anapiga shuti kali lakini Dihile anapangua, mabeki JKT wanaokoa na kuwa kona. Lakini haina matunda
Dk 87, Yanga wanaonekana kuridhika na bao tatu, wanaanzia kwa kipa Barthez, wanagonga taratibu wakionyesha kujiamini
Dk 86 JKT wanapata kona, anaichonga Mussa Juma inatua kichwani mwa Kamuntu na kuwa goal kick
Dk 83 hadi 85 JKT wanandelea kupiga pasi nyingi ambazo hakika hazina madhara
Dk 81, Msuva anaingiza krosi safi langoni mwa Yanga lakini Nonga na Mwashiuya wanajichanganya
DK 79, Pius anapiga krosi safi kabisa. Lakini Twitte anaokoa, anaosha mbele
Dk 72, Niyonzima anatoa pasi nzuri kwa Telela anapiga shuti kali linazuiwa na kuwa kona, lakini haina matunda
Dk 66 hadi 70, JKT wanagongeana zaidi lakini hakuna mashambulizi hatari kwenye lango la Yanga. Hali ya hewa ni nzuri hapa uwanjani na inaonekana inasaidia wachezaji kutochoka sana.
Dk 65, Kamuntu anaingia ndani ya lango la Yanga lakini anapiga shuti zembe kabisa
GOOOOOO Dk 63, Ngoma anaruka juu na kuifungia Yanga bao kwa ulaiiniii bada ya kuwazidi mabeki wa JKT
Dk 60, shuti la Kamuntu linangonga Bossou kichwani, sasa yuko chini anatiwa lakini mwamuzi anasema ni kona
Dk 55, JKT faulo, nje ya 18 ya Yanga inachongwa vizuri na Michael Aidan lakini Barthez anadaka kama nyani
Dk 51 Nonga anatoa pasi safi kabisa kwa Msuva, yeye na kipa anateleza
Dk 46, Yanga inamtoa Malimi Busungu anaingia Paul Nonga kuchukua nafasi yake
MAPUMZIKO
DAKIKA 6 ZA NYONGEZA
Dk 45, Mussa Juma akiwa nje ya eneo la 18 la Yanga anapokea pasi ya Naftal, lakini anapiga shuti kuuubwaaa
GOOOOO dk 43, Yanga inaandika bao la pili kupitia Gaba baada ya pasi nzuri kabisa ya Msuva aliyepewa pasi na Niyonzima
Dk 39 Barthez anampiga chenga kipa mshambuliaji wa JKT lakini anabaki na mpira, nusura asavabishe hatari
Dk 38 Dihile anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Ngoma baada ya kona nzuri iliyochongwa na Gaba
Dk 35, Mwaikimba anamtoka Juma Abdul anawahi na kuutoa, mpira unakuwa kona
KADI Dk 34 Emmanuel Pius analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Ngoma
Dk 31, krosi safi ya Ngoma inatua mguuni mwa Msuva, lakini anashindwa kufunga
Dk 29, JKT wanapata kona na Mussa Juma anakwenda kuichonga lakini haina faida
Dk 24 Issouf Gaba anapiga mpira mzuri lakini kipa Dihile anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona
Dk 21, Mwaikimba anaingia vizuri katika eneo la Yanga, lakini anakuwa hana kasi
Dk 16, Emmanuel Pius anapewa pasi nzuri na Kamuntu, lakini anapaisha juuu
Dk 15, Msuva anaingia na kumpa pasi nzuri Niyonzima lakini anapiga juuu
GOOOOOO Dk 11 Msuva anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya kuuchop mpira kwa uzuri kabisa.
Dk 3 hadi nne, timu zinaonekana kucheza zaidi katikati ingawa Yanga ndiyo wanaofika mara nyingi zaidi kwenye lango la JKT
0 COMMENTS:
Post a Comment