February 29, 2016





Simba imetangaza kumsimamisha nahodha wake, Hassan Isihaka baada ya kudaiwa “kumtemea mbovu” kocha wake Jackson Mayanja.

SALEHJEMBE imewambiwa kwamba, Mayanja ambaye alimuacha katika kikosi chake beki huyo wakati Simba ilipoivaa Yanga, aliamua kumpanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.

Inadaiwa, Isihaka baada ya kuambiwa atacheza, mbele ya wachezaji wenzake, alimuuliza Mayanja hivi: 

“Kwani likizo yangu ya kukaa benchi imeisha lini, uliona siwezi kucheza na Yanga, ila naweza kucheza leo.”


Inadaiwa, kauli hiyo inaelezwa kuwashangaza wengine, lakini Mayanja akaamua kuachana naye na kumpanga  Lufunga, beki mpya aliyejiunga wakati wa dirisha dogo akitokea African Sports. Simba ilishinda kwa mabao 5-1 na kutinga robo fainali.

2 COMMENTS:

  1. Tatizo viongozi wanakurupuka, huyo bado ni bwana mdogo na inaswezekana Mayanja ameshindwa kutengeneza upendo ndani ya timu kiasi kwamba mtu akikaa benchi anaonekana ana matatizo. Ni suala la kumuandaa kipsychology tu!! Kumfungia wakati utamfungulia ni kumfanya kuwa nunda, kwa maana nyingine humjengi bali unambomoa!! Je Mayanja angerushiwa jezi kama alivyofanya Costa kwa Mourinho si ndo angefukuzwa kwenye timu kabisa? Mbona Yanga akina Tambwe, Ngoma, Telela, Niyonzima wanawekwa benchi na wanaelewa!? Ni suala tu la mwl kuwaandaa psychologically wachezaji na kuwaonyesha kuwa kuwekwa benchi ni kupumzishwa au kuwapa nafac na wenzio wacheze ili wewe uliyepumzishwa uje na nguvu mpya na sio kwamba ni kushuka kiwango

    ReplyDelete
  2. huyu Mayanja anapanga timu kwa kukariri ona anavyomweka Manyika benchi hata kwa mechi za shirikisho anaua vipaji kwa wachezaji na kupunguza kujiamini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic