February 3, 2016


Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amewataja wanaume 11 ambao wataipa timu hiyo ubingwa msimu huu.
Simba wapo nyuma ya Yanga kwa pointi tatu na wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michezo iliyobaki msimu huu.

Huku leo Simba wakitarajiwa kucheza mchezo mgumu dhidi ya Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha wanarejesha heshima na kulisaka taji hilo walilolikosa misimu minne sasa, Mayanja amefunguka kuwa tayari amepata kikosi cha maangamizi.

Hata hivyo, Mayanja alisema licha ya kupata kikosi tegemeo, bado safu ya kiungo cha pembeni (wingi) inamvuruga akili mpaka sasa kwani hajapata mtu sahihi wa kumtegemea kama zilivyo nafasi nyingine.

 “Tayari kikosi cha kwanza ninacho, kama umeangalia mechi mbili zilizopita utajua hilo, lakini hiyo haimaanishi siwezi kuwabadilisha ila siyo mabadiliko zaidi ya wachezaji wawili. Wakati mwingine wanaweza kuwa majeruhi lazima ufanye mabadiliko lakini kikosi hakibadiliki sana” alisema Mayanja na kuongeza;

“Sema mpaka sasa bado sijapata mtu tegemeo kwenye wingi ya kulia, ukiangalia nimewajaribu Peter Mwalyanzi, Hija Ugando na hata Joseph Kimwaga, kwenye wingi ya kushoto naamini Brian Majwega, anaweza kuwa mtu sahihi, sema tatizo lake amekuwa majeruhi sana.”

Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ licha ya kuwa nje lakini ndiye beki kushoto chaguo la kwanza ambapo nafasi yake imekuwa akikaimu Abdi Banda kama Mwinyi Kazimoto anavyomshikia nafasi Majwega kwenye wingi ya kushoto.


Kulingana na kauli yake, jeshi la maangamizi la Mganda huyo liko hivi; Vincent Angban, Hassan Kessy, Tshabalala, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza, Danny Lyanga na Majwega. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic