February 3, 2016

CANNAVARO

Winga wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila amesema pamoja na kukosekana kwa wachezaji kadhaa bado timu hiyo ni ileile.

Hofu imeanza kutanda Jangwani kutokana na kikosi hicho kuwakosa mabeki tegemeo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani ambao wako nje kwa sababu tofauti na huenda ukawa mwanzo wa kuvurunda kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara.

Cannavaro anauguza jeraha la enka, wakati Yondani anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.

LUNYAMILA

Hata hivyo, Lunyamila anaamini Yanga bado ni ileile licha ya kutokuwepo kwa wawili hao ambao wamekuwa na pacha nzuri katika beki ya kati.

Lunyamila alisema bado Yanga ina kikosi kipana ambapo kuna watu wengi wenye uwezo wa kuziba nafasi zao.
“Bado wana Mbuyu Twite, Pato Ngonyani na Vincent Bossou, wanaweza kuiongoza timu. Sawa, ukizungumzia umuhimu wao ni mkubwa lakini sioni pengo kubwa ambalo linaweza kuwatoa mchezoni.


“Bahati nzuri Twite na Pato wamewahi kucheza nafasi hizo. Muhimu ni kutoruhusu kuumizwa na matokeo yaliyopita, wachukulie matokeo ya kawaida,” alisema nyota huyo ambaye ni mchambuzi wa gazeti hili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic