Kweli Jerry Muro ni shidaaa! Sasa ameibuka na jina jipya dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.
Awali aliwapachika jina la "Wamchangani", lakini safari hii ameamua kuwaita "Wamatopeni."
Msemaji huyo wa Yanga, amesema Simba hawastahili hata kuitwa wa "Mchangani".
"Unajua wakati tulipowafunga mara ya kwanza, waliona kama tumewabahatisha. Sasa tuliona vizuri kuwafunga tena.
"Ilikuwa kipigo na kurudia idadi ileile, hawa jamaa kila siku nawaita "Wamchangani" lakini safari hii hawa bora tuwaite "Wamatopeni", alisema Muro akionyesha mbwembwe kutokana na ushindi huo.
Yanga iliishinda Simba bao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, jana na kuhitimisha vipigo mara mbili msimu huu.







0 COMMENTS:
Post a Comment