| UWANJA WA KAITABA... |
Uwanja wa Kaitaba unakaribia kukamilika, timu ya Kagera Sugar imetoa onyo mapema kwa timu za ligi kuu kuwa zisitegemee kuondoka na pointi hata moja pindi Kagera itakaporejea kwenye uwanja huo.
Kaitaba upo kwenye hatua za mwisho kukamilika ambapo mafundi wanamalizia kumwaga mchanga maalumu kwenye nyasi, zoezi ambalo litachukua siku 10 kukamilika na kuwa tayari kwa kutumika.
| KAGERA |
Kocha wa Kagera, Adolf Rishard ambaye timu yake imekuwa ikihamahama viwanja tangu kuanza kwa matengenezo hayo, amenukuliwa akitoa majigambo hayo juzi kisha akaongeza:
“Kucheza Kambarage (Shinyanga) tunajihisi tupo ugenini japo ndipo tunapopatumia kama uwanja wetu wa nyumbani, tukirudi Kaitaba kila atakayekuja ajue kuwa hawezi kuondoka hata na pointi moja.”







0 COMMENTS:
Post a Comment