February 3, 2016


Aliyekuwa Kocha wa Simba, Dylan Kerr, raia wa Uingereza ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini akifanya kazi za kujitolea, ameshangaa kusikia mechi tatu za Azam zimesogezwa mbele.

Kerr, Januari 12, mwaka huu alifungashiwa virago ndani ya Simba sambamba na kocha wa makipa, Mkenya, Iddi Salim, kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo, ambapo tangu Mzungu huyo aondoke nchini, amepiga kambi Sauz kwa mapumziko marefu kabla ya kwenda nyumbani kwao.

Kerr amesema kwa sasa anafanya kazi ya kufundisha soka nchini Afrika Kusini kwa kujitolea akiwa na baadhi ya makocha wengine wa nchi hiyo, lakini wiki ijayo anatarajia kwenda Uingereza kuangalia mustakabali wa nini cha kufanya.

“Nipo huku Afrika Kusini nikifanya kazi na baadhi ya makocha wa hapa, tukifundisha mchezo wa soka kwa kujitolea huku tukisubiri hatma yetu kwani kuna uwezekano wa kupata timu za kufundisha hapa.


“Nimesikia Azam mechi zake mbili za ligi zimepelekwa mbele, kwa kweli nimeshangazwa na hili, siyo kitu kizuri, lakini nadhani kati ya timu zote, Simba ina nafasi kubwa ya kuwa bingwa kutokana na mechi zake nyingi kucheza nyumbani katika mzunguko huu wa pili,” alisema Kerr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic