February 23, 2016


Kampuni ya Multichoice Tanzania imekuja na habari njema kwa watumiaji wa ving’amuzi vyake vya DStv kwa kuzindua chaneli mpya za michezo zilizowekwa kwenye kifurushi maalum kwa ajili kuwafikia wateja wake wote.

Chaneli hizo murua zitakazotambulika kama SuperSport 11 na SuperSport 12 zimezinduliwa rasmi leo kupitia kifurushi kipya cha Compact ambacho sasa kitapatikana kwa Sh 84,500 lakini kwa upendeleo wa mteja mpya atakayenunua king’amuzi hicho atazawadiwa ofa ya bure ya kifurushi cha Compact kwa muda wa mwezi mmoja.


Akifafanua kuhusiana na hilo, Kaimu Meneja Mkuu wa DStv, Francis Senguji ameongeza kuwa chaneli hizo zinakuja na utamu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya England, Ligi Kuu ya Hispania pamoja na michuano ya Mataifa ya Ulaya 2016.

“Ni katika kutambua hali na nyakati ngumu ya kiuchumi tuliyonayo kwa sasa, tunaelewa pia mahitaji ya wateja wetu na kwa kuzingatia hilo tumeamua kuwasogezea karibu ligi kubwa za Ulaya za England na Hispania kupitia kifurushi cha Compact kinachopatikana kwa 84,500 tu.


“Hiyo inakwenda sambamba na mteja mpya atakayenunua king’amuzi kipya kwa 79,000 tu na kupata ofa ya kifurushi cha Compact kwa mwezi mzima na kuendelea kufurahia huduma zetu zinazopatikana Tanzania nzima.

“Ligi Kuu England itakuwa inapatikana kwenye SuperSport 11 na ile ya Hispania itakuwa inaonekana kupitia SuperSport 12 lakini pia michuano ya Euro 2016 inayosubiriwa kwa hamu nayo itapatikana kupitia chaneli hizo,” alisema Senguji.


Endapo utafanikiwa kuchukua kifurushi hicho mapema faida za awali unazoweza kufaidika nazo kwenye soka ni pamoja na kushuhudia mechi kali za wikiendi hii kule Uingereza kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal, Leicester City na Sunderland na mingine mingi.


Lakini Hispania pia kutakuwa na ‘game’ kali kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid wakati Barcelona ikivaana na Sevilla na Valencia inayoongozwa na Gary Neville itaingia dimbani kupambana na Athletic Bilbao. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic