February 18, 2016



Na Mohammed Issa, Morogoro
Kocha Jackson Mayanja anajua wanachotaka wao ni kuwapiga Yanga, na safu yake ya ushambulizi ndiyo yenye kazi ya kumaliza mchezo.

Hivyo amekuwa akitumia muda maalum kuwafua washambuliaji wake wanaoongozwa na Hamisi Kiiza, kwamba inawezekana kuwamaliza Yanga.

Katika kambi ya Morogoro ambayo sasa kuingia imekuwa shida wakati wa mazoezi ya Simba, pamoja na kufundisha mazoezi mengine, Mayanja amekuwa akiwanoa washambuliaji wake, akionyesha kuwaongezea mbinu.

Simba ina mabao 35 ya Ligi Kuu Bara, huku Yanga ikiwa imefunga 42. Lakini muhimu zaidi ni kufunga mabao katika mechi ya Jumamosi.

Mazoezi anayowapa wachezaji wake ni pamoja na kkupiga mipira ya vichwa, mashuti na umaliziaji wa kiufundi.


Lakini alikuwa akiwapa mazoezi ya kuhakikisha wanakuwa watulivu wanapoingia katika enero la 18 la Yanga ili kuwa na uhakika katika umaliziaji.

Hata kabla ya Simba kuweka kambi mjini Morogoro, Mayanja alikuwa akiwanoa washambuliaji wake kwa mazoezi maalum kwenye Uwanja wa Boko Veterani, hali inayoonekana kuwasaidia na wanafanya vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic