February 18, 2016

YANGA WAKIWA MAZOEZINI MJINI PEMBA, JANA

Na Mariam Mohammed, Pemba
Benchi la ufundi la Yanga sasa limeamua kufanya mazoezi ya siri bila ya wengine kuona nini kinachoendelea.

Yanga ipo kambini mjini hapa kujiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, keshokutwa Jumamosi.

Kuanzia jana, Yanga imeamua mazoezi yake kuanzia hatua fulani kufanyika bila ya kuwepo kwa watu wengine wasio wahusika kwenye Uwanja wa Gombani,.

Mashabiki, hata Waandishi mbalimbali wa habari, wamefukuzwa katika mazoezi ya Yanga ili Kocha Hans van Der Pluijm aendelee na “mambo yake”.


Awali, siku mbili za mwanzo, mashabiki na waandishi walipewa nafasi ya kuona mazoezi hayo. Lakini kuanzia jana, mazoezi mwanzoni wanaweza kuruhusiwa lakini baada ya muda watu hutakiwa kutoka nje ya uwanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic