February 17, 2016

AZAM FC
Kipigo cha bao 1-0 walichokipata Azam FC dhidi ya Coastal Union kimewaongezea morali na nguvu Yanga ya kutokubali kupoteza mchezo na badala yake kushinda mechi zote za Ligi Kuu Bara ikiwemo dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

Azam wikiendi iliyopita ilipoteza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao likifungwa na beki wa zamani wa Simba, Miraji Adam.

PLUIJM
Matokeo hayo mabaya ya Azam, yamepokelewa kwa furaha na Yanga kutokana na wapinzani hao kubaki kwenye nafasi hiyo ya tatu wakiwa na pointi 42 nyuma ya Simba yenye 45 na Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 43.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, alisema kupoteza mechi kwa Azam kumewapa changamoto ya wao kufunga kila mechi watakayokutana nayo kwenye ligi kuu.

Pluijm alisema, kikubwa wanachokiangalia wao ni ubingwa pekee ambao utatokana na matokeo mazuri ya kila mechi kwa kuanzia na mechi dhidi ya Simba ili wawaache wapinzani wao Azam wanaochuana kwenye mbio za ubingwa.

“Matokeo ya Azam kupoteza mechi dhidi ya Coastal yametupa morali na nguvu ya sisi kutokubali kupoteza mechi zote zilizobaki za ligi kuu, hivyo tunataka tushinde kila mchezo kwa kuanzia na mechi ya Simba.


“Kinachotakiwa hivi sasa ni kushinda michezo yetu yote ili turejee kwenye kilele cha msimamo wa ligi kuu na hilo litawezekana baada ya kushinda kila mchezo wetu, hiyo ni baada ya Azam kupoteza mchezo wake dhidi ya Coastal,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic