February 17, 2016


Na Mwandishi Wetu, Pemba
Mashabiki wa Yanga Kisiwani Pemba, wameanza kukumbwa na hofu kubwa baada ya majeruhi kuanza kuiandama timu hiyo iliyopiga kambi yake kisiwani hapa.

Yanga iliwasili hapa Jumapili iliyopita kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wao wa jadi Simba, utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Mashabiki hao wamesema hatihati ya kukosekana kwa Juma Abdul na Simon Msuva katika mchezo huo, litakuwa ni pigo kubwa kwa Yanga na kuna hatari ya kupoteza mchezo huo.
Hofu hiyo imekuja baada ya juzi jioni wachezaji hao kushindwa kufanya mazoezi na kubaki nje ya uwanja wakitazama wenzao wakiendelea kujifua.

Kutokana na hofu hiyo, mashabiki hao walimtaka daktari wa timu hiyo, Nassor Matuzya, kuhakikisha anafanya kila njia ili wachezaji hao waweze kupona haraka na kurudi katika hali yao kama zamani na kuweza kucheza dhidi ya Simba.

Championi Jumatano lilitaka kufahamu majeraha ya wachezaji hao yatakuwa ni muda gani, lakini Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema uongozi umekataza kutolewa kwa taarifa zozote juu ya maendeleo ya kambi yao kisiwani hapa.

Huku meneja huyo akigoma kutoa ushirikiano vizuri, lakini mmoja kati ya viongozi waliofuatana na timu hiyo, alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini na kusema majeraha ya wachezaji hao yametokana na mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim walioshinda bao 1-0.


Alisema hata Salum Telela naye ni majeruhi, lakini anafanya mazoezi na wenzake, hali inayoifanya kambi hiyo hadi sasa kuwa na wachezaji watatu majeruhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic