February 10, 2016


PETER MANYIKA
Kipa Peter Manyika ameumia enka baada ya kukanyangwa, uongozi Simba umethibitisha.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amezungumza na SALEHJEMBE na kusema Manyika alikanywagwa, lakini kwa sasa anaendelea vizuri.

“Kweli Manyika aliumia lakini ni kidogo tu. Kwa sasa anaendelea vizuri kabisa na matumaini makubwa hadi Jumamosi atakuwa vizuri kabisa,” alisema Manara.

Simba inashuka dimbani Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kuwavaa wenyeji wake Stand United.

Stand ambao wamekuwa wagumu kwa Simba, nao wamejiandaa tayari kwa mechi hiyo.


Lakini Manara amesema kikosi chao kipo tayari kabisa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajia kuwa na mvuto wa juu kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic