Tiketi za Sh 7,000 katika pambano la Yanga dhidi ya Simba kesho, limezua zogo kubwa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki zaidi ya 100 walianza kulalamika wakida kuna mchezo mchafu kwamba tiketi hizo zimeisha kwa kuwa kuna ulanguzi unafanyika makusudi.
Mashabiki hao wameiambia SALEHJEMBE kwamba tiketi hizo zimeuzwa kwa saa moja pekee, jambo ambalo wanaamini TFF itakuwa inafanya ujanja.
“Haiwezekani tiketi ziishe ndani ya saa moja. Wanafanya makusudi baadaye watuuzie kwa bei kubwa. Hatukubaliani na hili kwa kuwa sisi watu wa chini tunaumia,” alisema Ibrahim Mohammed, mmoja wa mashabiki waliokuwa wamekosa tiketi.
Kufikia saa 4 asubuhi, tiketi za Sh 7,000 zilikuwa zimeisha kila sehemu, hali iliyosababisha mzozo huo.







0 COMMENTS:
Post a Comment