Mechi tano za kila timu kati ya Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid zitakwua zimeamua nani ni bingwa wa La Liga.
Kila mmoja, inategemea atazicheza vipi karata zake. Barcelona inaonekana kuwa na nafasi nzuri kwani katika mechi tano zinazokuja haina mechi dhidi ya Madrid wala Atletico.
Lakini Atletico na Madrid zitakutana na zitakuwa katika wakati mgumu wa kuhakikisha zinautumia vizuri mchezo huo.
Barcelona ipo kileleni ikiwa na pointi 60, tofauti ya pointi saba na Real Madrid yenye pointi 53 katika nafasi ya tatu na Atletico na 54 katika nafasi ya pili.
Kama itashinda mechi zote tano zijazo, basi itakuwa ni vigumu kuhakikisha timu hizo nyingine mbili zinakamata.
MECHI TANO ZIJAZO ZA BARCA:
Las Palmas vs BARCELONA – Feb 20
BARCELONA vs Sevilla – Feb 28
Rayo Vallecano vs BARCELONA – Mar 3
Eibar vs BARCELONA – Mar 6
BARCELONA vs Getafe – Mar 12
MECHI TANO ZIJAZO ZA ATLETICO:
ATLETICO vs Villarreal – Feb 21
Real Madrid vs ATLETICO – Feb 27
ATLETICO vs Real Sociedad – Mar 1
Valencia vs ATLETICO – Mar 6
ATLETICO vs Deportivo – Mar 12
MECHI TANO ZIJAZO ZA MADRID:
Malaga vs REAL MADRID – Feb 21
REAL MADRID vs Atletico – Feb 27
Levante vs REAL MADRID – Mar 2
REAL MADRID vs Celta Vigo – Mar 5
Las Palmas vs REAL MADRID – Mar 13








0 COMMENTS:
Post a Comment