February 2, 2016

RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA (KULIA) WAKATI WA UZINDUZI WA DUKA HILO. KUSHOTO NI IMANI KAJURA, MKURUGENZI MTENDAJI MKUU WA AIG.

Baada ya kufungua duka ambalo litakuwa likiuza vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu, Simba sasa ina mpango wa kufungua duka klabuni.

Makao makuu ya Simba yako katika barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam ambalo ni eneo katikati ya Kariakoo, kitongoji cha kibiashara katika jiji hilo la pili kwa ukubwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema baada ya duka hilo kwenye jumba la biashara la Dar Free Market, sasa wanaangalia kufungua jingine.

“Tunaanza mchakato kwa ajili ya kufungua duka pale klabuni, mashabiki. Wanasimba ambao watakuwa na uwezo na nia, pia tunawakaribisha ili kuwapa tenda,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic