Azam FC wamesema wanajua ugumu wa mechi inayofuatia ya Kombe la Shirikisho na kuahidi watajiandaa vizuri zaidi.
Azam FC itakutana na Esperance ya Tunisiai ambayo mara ya mwisho ilikutana na timu za Tanzania mwaka 2009.
Esperance iliitoa Yanga kwa kuifunga jumla ya mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa jijini Tunis.
Azam FC itaanzia nyumbani kati ya Aprili 8 na 10 na marudio jijini Tunis yatakuwa ni kati ya Aprili 19 hadi 20.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga maarufu kama mbunifu amesema wanajua ugumu wa mechi hiyo.
“Itakua mechi ngumu, kila unavyopanda juu unakutana na timu imara zaidi. Tunalijua hilo na Azam FC ambao ni mwakilishi wa Watanzania katika michuano hiyo, itajiandaa vizuri,” alisema.
Azam FC imefanikiwa kuvuka na kufika katika hatua hiyo kwa kuitwanga Bidvest ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3.
0 COMMENTS:
Post a Comment