Aliyewahi kuwa Kocha wa Makipa wa Simba, Iddi Salim amesema maisha yanakwenda vizuri kabisa katika klabu yake mpya ya MFK Topolcany ya nchini Slovakia.
Akizungumza na SALEHJEMBE moja kwa moja kutoka mjini Bratislava, Slovakia, Iddi raia wa Kenya alisema ameanza kazi hiyo na anajifunza mengi.
“Mambo mengi yako katika mpangilio na yanakwenda kwa wakati. Nafurahia lakini najifunza pia,” alisema kocha huyo wa zamani wa Kenya, Harambee Stars.
Iddi alitimuliwa na uongozi wa Simba ulipoamua kumuondoa aliyekuwa kocha Mkuu, Dylan Kerr na nafasi ya kuchukuliwa na Jackson Mayanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment