March 22, 2016


Jua linaonekana kuwa tatizo kubwa kwa Taifa Stars inayojiandaa kuivaa Chad ikiwa nyumbani kesho.

Stars itaivaa Chad katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika. Mechi hiyo itapigwa jijini N'Djamena.

Mratibu wa Taifa Stars, Msafiri Mgoyi amesema jua ni kali, pia hali ya hewa ya joto ipo juu sana.

"Nyuzijoto zinafikia hadi 40, si kawaida. Hali ya hewa kwa kweli ni ya joto lakini makocha wamekuwa wakilifanyia kazi hilo na mazoezi yetu yalikuwa mchana," alisema Mgoyi.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwasa yeye amesema hali hiyo imekuwa ngumu kidogo lakini wanajua wanachofanya na watapambana.

"Kweli hali ya hewa ni joto sana. Nasi tumekuwa tukifanya mazoezi wakati wa jua kali ili kuizoea hali hii kwa kuwa nao wameamua mechi hiyo icheze mchana wa jua kali," alisema Mkwasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic