March 22, 2016


Kiungo wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid ni kati ya wanasoka ambao wamekuwa mfano katika suala la kujali familia zao.

Shekhan mara nyingi amekuwa kazini katika jiji la Stockholm nchini Sweden anakoendesha maisha yake.

Kama atakuwa nje ya kazi, basi ni mtu wa familia na anaonekana kuwa mmoja wa watu wanaotoa nafasi kubwa kwa familia yake.

Picha nyingi anaonekana ni mzazi mwenye upendo kwa watoto wake kama hii ambayo yuko na binti yake akicheza naye.


Shekhan ni kati ya viungo bora ambao Tanzania imewahi kuwa nao na aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa akisaidiana na Selemani Matola aliyekuwa kiungo wa ukabaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV