KIONGERA |
Mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera ameanza mazoezi na sasa anaanza kuonekana yuko vizuri.
Kiongera ameanza mazoezi leo ni siku ya tatu akiwa amerejea mazoezini baada ya kusumbuliwa na kuchanika kwa nyama za paja.
Kawaida, nyama za paja huwa hazina tiba kuu zaidi ya kupumzika huku mhusika akitumia dawa za maumivu.
Kiongera ambaye alisajiliwa na Simba msimu uliopita kisha kupelekwa kwa mkopo KCB ya Kenya na kurudishwa katikati ya msimu huu hajaonyesha kiwango kizuri mpaka hivi sasa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Raia huyo wa Kenya, Juzi Jumatatu, alianza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzake yaliyofanyika kwenye Ufukwe wa Coco, na jana Jumanne alifanya mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Boko Veteran, jijini Dar.
Leo ni siku ya tatu na Meneja wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ anaamini yuko fiti na kocha Jackson Mayanga ndiye uamuzi wa mwisho kuhusu kumtumia.
0 COMMENTS:
Post a Comment