March 22, 2016


Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche anashika nafasi ya pili kwa upachikaji mabao katika michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea.

Kipre raia wa Ivory Coast amefunga mabao manne sawa na Amr Barakat wa Misr El Makasa ya Misri na Rafael Manuvire wa Harare City ya ZImbabwe ambaye imeishang’olewa katika michuano hiyo. 

Kinara wa upachikaji mabao katika michuano hiyo ni Love anayekipiga katika klabu ya Sagrada Esperanca ya Angola.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao matatu, hat trick katika mechi ya pili dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV