March 10, 2016

DHAIRA BAADA YA KUANZA KUUGUA AKIWA NA KOCHA WAKE, JOHANNSSON.

IBV Vestmannaeyjar ya Iceland, Bjarni Jóhannsson amemuombea kipa wake, Abel Dhaira aliyegundulika kuwa na kansa ya utumbo.

Jóhannsson amesema klabu ya IBV itapitisha harambee kupitia uongozi wake ili kumsaidia Dhaira kupata fedha kwa ajili ya matibabu.

Dhaira aliwahi kuichezea Simba ikiwa chini ya Kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa, hata hivyo hakufanya vema sana. Dhaira ni mtoto wa kipa nyota wa zamani wa Uganda, Bright Dhaira.

Pamoja na harambee hiyo, Jóhannsson  amesema: “Ni jambo la kusikitisha, linaumiza na kushitua. Lakini bado tuungane kumuombea Abel ambaye alikuwa mpambanaji.

“Kama mwalimu, pamoja na wachezaji, klabu kwa ujumla tumekuwa naye pamoja katika kipindi chote cha wakati mgumu wa kuugua akiwa hapa Iceland na baadaye aliporejea Uganda. 

“Tunawaomba wadau wote wa soka tuungane ili kumuombea na kumsaidia Abel ambaye sasa anateseka.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic